Ujue Mtindo wa Uandishi wa Utambaji
Kujua tofauti ya mitindo ya uandishi inakusaidia kuwa bora zaidi kwenye uandishi hasa kugundua upekee wako wa kumnasa msomaji wako afurahie kazi yako uliyoandika. Swali la kwanza kujiuliza kabla ya kuandika ni “Kwanini naandika kazi hii? Je! Ni kuelezea, kufafanua, kufundisha, kushawishi au kuburudisha?”. Mojawapo ya mitindo minne ya uandishi ni uandishi wa utambaji.
Mtindo wa uandishi wa utambaji
Huu ni uandishi wa hadithi au hekaya. Ni mtindo wa masimulizi. Muandishi unatengeneza kisa na kuwaumba wahusika. Ni mtindo wa uandishi unaojibu swali la “Nini kilitokea”. Sifa za mtindo huu wa uandishi ni;
- Muandishi anasimulia
- Kuna kisa na wahusika
- Kuna mwanzo wa kisa na mwisho wake
Mfano wa kazi za uandishi unaofuata mtindo huu ni; Hadithi, Tawasifu, Wasifu na n.k. Mfano, “Sitaki uongo wako” alisema Suzy.
________