Tabia 5 zinazoleta mafanikio kwa muandishi
Kila muandishi wa vitabu hutaka kufanikiwa lakini mafanikio huchagizwa na tabia anazokuwa nazo muandishi mwenyewe. Kuna tabia tano ambazo muandishi akiwa nazo basi mafanikio huja yenyewe.
1. Andika kila siku. Kuandika kila siku si jambo
dogo na pengine wajiuliza, “hili linawezekanaje?”. Lakini unaweza kutenga
dakika 5 mpaka 10 kila siku ukaandika, hata kama ni kitu kidogo kiandike.
Unaweza kuwa na dakika hizo asubuhi, usiku au mchana wakati. Misuli yako kama
muandishi hupashwa kila siku unapoandika.
2. Soma kadri unavyoweza. Huwa wanasema muandishi
mzuri ni msomaji mzuri. Soma vitabu vya waandishi mbalimbali, hata vile ambavyo
sivyo vya aina unayooandika wewe. Unapofanya hivyo unapata ladha mbalimbali za
waandishi wengine na itakufanya kuwa bora zaidi
3. Jiwekee malengo yaliyo wazi. Utapimaje mafanikio
yako kama huwezi malengo? Weka malengo yaliyo wazi, yanayopimika.Unaweza
kutimiza malengo unayojua, na ambayo unaweza kujikumbusha.
Soma pia: Ufanye Nini Uzinduzi Wa Kitabu Chako Unapofeli?
4. Penda kutumia teknolojia. Muandishi lazimia
ujenge tabia ya kwenda na teknolojia. Si muda wote utatumia Microsoft Word
kuandika, nenda playstore au appstore na weka evernote. Huwezi kutembela na
kalenda kila mahali ili kujikumbusha malengo yako, jizoeze kutumia google
kalenda. Zipo teknolojia nyingi mno, jizoeze kuzitumia.
5. Maliza kila unachoanza. Uwe na tabia ya kumalizia vitabu unavyoandika. Najua ni ngumu hii, lakini inawezekana. Kumbuka nguvu uliyoweka ulipoanza kuandika, ukiishia njiani umepoteza muda na nguvu yote uliyoweka.
Tembelea HAPA kusoma kozi za uandishi wa vitabu bila gharama yoyote