#KitabuKipya | Muhtasari wa kitabu cha jinsi ya kutunza muujiza
Lengo kuu la Yesu Kristo kuja duniani na kufa msalabani nikumlejesha mwanadamu kwenye ile nafasi ya awali baada ya anguko la mwanadamu wa kwanza Adamu kwahiyo muujiza mkuu kuliko yote aliokuja kuufanya Yesu hapa duniani ni kuleta WOKOVU na ndio kitu cha thamani kuliko vyote hapa duniani yaani (lulu) na kitabu hiki kitaenda kukufafanulia muujiza huu mkubwa na wa kwanza anaopaswa kuupokea mwanadamu
Roho Mtakatifu amenipa
neema kukuletea kitabu hiki, kilichopo mikononi mwako sasa, ili kupata siri
zilizofichika ndani ya muujiza wa wokovu
na miujiza mingine ili usiupoteze maana umepata kitu cha thamani kutoka kwa
Mungu kuliko kitu chochote duniani kwahiyo ninakushauri fatilia kitabu hiki
mpaka mwisho pasipo kupuuza maana ni ufunuo niliofunuliwa na Roho Mtakatifu
kutoka kwa Mungu aliye hai.
kwanza kabisa unatakiwa kugeuza fikra, fahamu na mawazo yako na kuelewa kuwa lengo kuu la Yesu Kristo kuja duniani na kufa msalabani si kukupatia gari, nyumba, kazi, fedha mme/mke n,k japo ni vizuri kuwa navyo na si dhambi ila agenda kuu ya Yesu Kristo kuja duniani nikukikomboa na kukilejesha kile kilichopotea (yaani sisi wanadamu tulio kuwa tumepotea) kupitia WOKOVU Yonana 3:16 “Kwa maaana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” Mathayo 18:11 “kwa maana mwana wa adamu alikuja kukiokoa kilichopotea”
Wewe unayesoma kitabu hiki
hakikisha usipitwe na neema hii ya wokovu maana ndio tiketi ya kukupeleka mbinguni
na ndio muujiza mkuu aliouachilia Mungu kuliko yote hakikisha umemkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na
Mwokozi wa maisha yako yaani UMEOKOKA na kitabu hiki kimebeba mafunuo
makubwa Muujiza ni kitu gani
Muujiza ni zawadi kutoka kwa Mungu, anayoipata mtu kwa kuomba au bila kuomba kwa hiyo kwa lugha nyingine muujiza ni neema anayoipata mtu kutoka kwa MUNGU kwa kupewa bure bila kulipia gharama yeyoyote ile, muujiza unaweza kuwa uponyaji, kazi,biashara, mtaji, kilimo, ufaulu katika masomo, mifugo,safari, huduma, kalama au kipawa, fedha n.k na ili uutunze muujiza wako Roho myakatifu ameyafunua mambo 11 ya jinsi ya kutunza muujiza wako na yanapatikana ndani ya kitabu hiki cha JINSI YA KUTUNZA MUUJIZA WAKO KILICHOANDIKWA NA; Mwinjilisti Vedasto Musolini Zimbeiya ambaye ni mtumishi wa MUNGU anaye hubiri na kufundisha neno la Mungu katika semina mbalimbali pasipo mipaka katika madhehebu yote anapoalikwa na yupo tiyari kuja kufundisha neno la Mungu mahali popote pale anapokaribishwa