[Hadithi fupi] Alisema nataka lakini...
Kama siku mbili tatu zilizopita kuna mzee mmoja hapa jirani na kwangu alimwona kijana mmoja anatembea huku macho kodo kwenye simu yake
Mzee akahamaki "hawa vijana na siku hizi hovyo kabisa, badala atembee anaangalia mbele yeye yuko busy na simu"
Yule kijana
alipokuwa kama anampita yule mzee akasimama na kumsalimia
"mzee wangu shikamoo"
"marhabaa, hujambo kijana"
"sijambo"
Akiwa na donge kooni akamuulize yule kijana, "mbona macho yako kwenye simu sana?"
Kijana akasema "nasoma kitabu kwenye simu"
"Aaarghh, kwenye simu? ndo unasomaje?" akauliza
Kijana akasema, "siku hizi kuna vitabu ambavyo unasoma tu kwenye simu tunaita ebooks, soge karibu nikuoneshe"
Akitikisa kichwa, mzee alisema nataka lakini...akaondoka bila kumalizia
__
Ndio ukiwa na simu yako au laptop yako unaweza kusoma vitabu bila stress. Nimekuandalia orodha ya vitabu kadhaa vya kuanza kusoma wikiendi hii.
NAANDIKAJE KITABU? | Kitabu hiki ni
toleo lililoboreshwa la kitabu cha Mbinu Rahisi Za Kuandika Kitabu.
Wakati nilipotoa kitabu cha Mbinu Rahisi Za Kuandika Kitabu nililenga
kuwasaidia watu wanaotaka kuingia kwenye uandishi wa vitabu lakini
hawana watu wa kushika mkono ili kufanikisha ndoto zao. Lengo bado ni
lile lile isipokuwa nimeboresha zaidi na kufanya marekebisho fulani
fulani baada ya kupokea maoni kutoka kwa wasomaji wengi waliosoma
kitabu. Katika toleo hilo jipya, nimeongeza vitu vingi ambavyo
naamini, unapokisoma kitabu hiki utatoka ukiwa na nguvu mpya ya
kuandika kitabu chako na hatimaye kutimiza ndoto yako ya kuwa
mwandishi wa kitabu. Naandikaje kitabu? Ni swali ambalo nimejibu
katika kurasa zinazofuata. Mimi naamini, kuandika kitabu ni ujuzi
ambao kila mtu anawez kujifunza. Anza kusoma!
> https://selar.co/lo21
MUDA NA WAZAZI | Wazazi ni dhahabu. Wazazi
ni nguzo ya mafundisho ya kila kijana. Hawa ndio walimu wa kwanza
katika maisha yako. Kupitia Muda na wazazi wako utajifunza jinsi ya
kutambua nyakati mbalimbali katika maisha yako. Wengi wameanza
kuwasahau, kuwadharau na kutojifunza kutoka katika maisha yao. Je,
unatambua nafasi ya kila mmoja katika familia? Kitu gani kimekuwa
kikikutenganisha na mzazi wako?. Baraka, Furaha na Amani
vimejificha kupitia muda na wazazi wako. Kupitia Muda na Wazazi
utajifunza jinsi ya kutambua nafasi ya kila mmoja katika familia na
kutoka hatua moja hadi nyingine. Utajifunza jinsi ya kuwa kijana
anayeheshimu na kuthamini kila hatua anavyopitia. Wekeza juu ya
wazazi wako. Usikubali kufanya makosa yanayowaumiza wengi. Kubali
kubadilika na uwe mwepesi wa kujifunza. Anza kusoma!
> https://selar.co/jvxc
TAKE CHARGE - A Guide to Unleash your Potential | aking
charge of your life is an important aspect that sustains individual
development. It helps you to control your life and steer it in the
desired direction. Unfortunately, many people do not take charge to
overcome their shortcomings and this tendency holds them back from
realizing their full potential. If you read this book thoroughly, you
will develop an understanding of how to overcome your shortcomings in
different areas and by applying the strategies provided. Read now
> https://selar.co/env7
INTENTIONS - A Novel from Tanzania | Ntayo
(the main character) is a visionary boy living in hard and chaotic
life situations whose intentions are to liberate himself and family
from the storms of poverty like other people wish to do in their
lives. His sister called Mwamini, works in a factory and she is the
one who fixes up all school costs for Ntayo, between the community
that lost faith in education by seeing thousands of unemployed youths
stamping all over streets joblessly. Read now
> https://selar.co/hg39
MFUKO WA DHARURA | Jifunze kuhusu fedha,
kuweka bajeti, fedhaza majanga na dharura. Kitabu hiki ni msaidizi
wako wa kufahamu mambo ya fedha. Anza kusoma!
| https://selar.co/oijm
Angalia vitabu zaidi
hapa. Karibu kwa maoni yako kwenye comments.