Kuwa mwandishi serious inataka nini?
Msomaji anaposoma kitabu cha mwandishi fulani huwa anakutana na mambo ambayo yatampa picha ya kumuona mwandishi yupo serious au la. Kwa bahati mbaya, wasomaji wengi wanapomwona mwandishi hayupo serious hubaki na dukuduku moyoni bila kumpa mwandishi mrejesho wa kitabu chake. Hii sio poa hata kidogo lakini ndio uhalisia wa mambo ulivyo
Mwandishi huonekana hayupo serious ikiwa atafanya makosa fulani fulani kuanzia kwenye kuandaa kitabu chake mpaka kitabu kinapofika kwa wasomaji.
Sasa,
Kuwa mwandishi serious inataka nini? Hili si swali jepesi lakini majibu yake yapo. Upo tayari kufahamu majibu yake? Kama ndio, nataka nikwambie jambo moja zaidi.
Nimeandaa mafunzo ya bure kwa waandishi wa vitabu ambayo yataanza Jumatatu ya 19.12.2022. Kwenye mafunzo haya nitafundisha kuhusu MAKOSA YA KUEPUKA ILI UWE MWANDISHI WA VITABU ULIYE SERIOUS. Kwa nini mafunzo haya? Nitakachofundisha itakuwa ni majibu ya swali “Kuwa mwandishi serious inataka nini?” na msukumo wangu ni wewe uonekane ni mwandishi uliye serious kwa watu ambao watashika kitabu chako na kukisoma.
Kinachofuata?
Najua sasa unajiuliza,
naingiaje kwenye mafunzo haya? Ni rahisi sana, nitafundisha kwenye group
la WhatsApp la Free DaudiPages Courses na bila kuchelewa jiunge sasa hivi hapa,
Utapata nini zaidi kwenye mafunzo haya?
Mbali ya kufaidika na mafunzo niliyoandaa ambayo ni bure, pia nitatoa ofa na bonasi kedekede kwa wote ambao watakuwa kwenye mafunzo haya. Ofa na bonasi hizi ni kwenye kozi za uandishi wa vitabu na vitabu vyangu nilivyoandika. Si tamu hii aisee!
See you 19.12.2022!