Vitabu vitatu vitakavyobadilisha maisha yako ya maombi kabisa
“Kitabu ni zawadi ambayo unaweza kuifungua tena na tena”, ni maneno yaliyosemwa na Garrison Keillor, mwandishi wa vitabu kutoka Marekani. Kila unapoifungua zawadi hii ya kitabu na kusoma tena na tena, maisha yako hayawezi kubaki vile vile, lazima utapiga hatua kuboresha maisha yako.
Kuna kundi kubwa la watu wanaopenda kuboresha na kubadilisha maisha yao ya maombi lakini hawajui waanzie wapi. Sasa, nimekuandali vitabu hivi vitatu ambavyo vitabadilisha maisha yako ya maombi kabisa.
1. JIFUNZE KUDUMU KATIKA MAOMBI. Jifunze kudumu katika maombi ni ujumbe unaotokana na msisitizo mkubwa katika neno la Mungu juu ya maombi au kuomba kwa kila mkristo, akiwa kama mtu binafsi lakini pia akiwa kama mwakalishi wa ufalme wa Mungu hapa duniani.
Maombi au kuomba ni suala la msingi sana kwa kila mkristo kwani maombi hudhihirisha asili, uhai, nguvu na mamlaka ya mtu mkristo. Zaidi maombi au kuomba huthibitisha mahusiano ya karibu kabisa kati ya mtu aliyeokoka na Mungu.
Bila shaka kupitia kitabu hiki msomaji atapata kujifunza mambo muhimu na ya msingi sana kuhusiana na wajibu na fursa ya thamani kabisa ya kuomba anayopewa mtu yeyote yule aliyeokoka na kuishi maisha yenye kuongozwa na Roho Mtakatifu.
Kitabu hiki ni eBook na kinapatikana hapa (bonyeza) na utakipata mara mojakwenye baruapepe yako.
2. MAARIFA JUU YA MAOMBI UNAYOTAKIWA
KUOMBA. Maarifa juu ya maombi unayotakiwa kuomba ni kitabu kinachoweza
msaidia mtu yeyote bila ya kujali hali yake ya kiroho. Kitabu hiki kinatoa
mwanga, maarifa pamoja na kutoa majibu ya maswali na mitazamo mbalimbali kuhusu
maombi yanayohitajika ili Mungu afanye kitu katika maisha yako ya kimwili na
kiroho pia.
Hii ni baada ya kufanya tathmini katika Roho Mtakatifu na kugundua kwamba iko idadi ya wakristo wengi wanaomba sana lakini si katika maarifa, hivyo kitabu hiki kitakuwa ni msaada mkubwa sana kwako ili uweze kuomba maombi yenye nguvu mbele za Mungu. Hosea 4:6a inasema "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;"
Kitabu hiki ni eBook na kinapatikana hapa (bonyeza) na utakipata mara mojakwenye baruapepe yako.
3. FAHAMU SABABU 101 KWANINI TUNAOMBA. Jinsi ya kufanikiwa katika maombi ni kitabu ambacho kitakuwezesha kufahamu: Maombi ni nini? Sababu 101 kwa nini tunaomba Aina 6 za maombi, Kanuni 10 za maombi yenye majibu, Sababu 25 za kutojibiwa kwa maombi, Faida 20 za maombi, , Hasara 10 za kutoishi maisha ya maombi, Kweli 75 kuhusu maombi, Sababu 14 kwa nini watu wengi wanashindwa kuomba, na Siri 9 za kukuwezesha kuomba kwa muda mrefu.
Kuna vitabu vingine vya kiroho zaidi ya 30+ vinavyopatikana hapa. Kuna baadhi ya vitabu vichache ambavyo vipo kwenye PUNGUZO KUBWA la bei, angalia hapa na chagua ambacho utapendakukisoma.