Mafunzo 10 kutoka kwenye kitabu cha Ushindi Katika Hali Ngumu
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema, “Ikiwa tutakutana na mtu mwenye akili adimu, tunapaswa kumuuliza anasoma vitabu gani”. Ukweli wa kauli hii ni kwamba mtu yeyote aliye tofauti anasoma vitabu. Mtu wa kawaida akipita kwenye nyakati ngumu anapigika vilivyo, lakini anayesoma vitabu huwa na mbinu za kuvuka hali ngumu.
Kitabu cha Ushindi Katika Hali Ngumu ni nyenzo yako ya kukusaidia unapopita katika nyakati ngumu, na tumekuandalia mambo 10 ambayo utajifunza ndani ya kitabu hiki. Mambo haya 10 ni kionjo tu kwako, kufahamu zaidi, kitabu hiki kinapatikana hapa.
Haya ndiyo mambo 10 kutoka kwenye kitabu cha Ushindi Katika Hali Ngumu.
- “Kama kwa Mungu hakuna jambo gumu la kumshinda na ikiwa tunamwendea yeye ili kutusaidia kutoka kwenye magumu; basi hakuna hali ngumu yoyote ya kuweza kutuzamisha na kutushinda”
- “Hali ngumu ni kifungashio cha nje tu cha mambo mazuri”
- “Wingi wa ndiyo siyo usahihi wa jambo; usitishwe”
- “Tunapitia hali ngumu ili kulipa gharama ya maamuzi ya hovyo tunayofanya kwa kuwasikiliza wengi wanasemaje”
- “Bora uchelewe kuliko kuwahi ikiwa unakoenda bado hujajiridhisha vya kutosha”
- “Raha ya kushinda changamoto ni kubwa kuliko raha ya kukosa changamoto”
- “Utamu wa stori si maneno bali ni ushindi kwenye magumu
- “Kaa kuanzia asubuhi mpaka jioni ukilalamika, ikifika jioni nitakuuliza swali rahisi, ‘umebadilisha nini ulivyomaliza kulalamika?”
- “Ukweli wa maisha ni kuwa unayemtegemea kukutoa wewe kwenye hali ngumu, yeye pia yuko katika hali ngumu yake”
- “Ushindi huanza na kutengenezwa toka ndani ya mtu ma si nje ya mtu”
Soma zaidi ya haya mambo 10, pakua kitabu cha Ushindi KatikaHali Ngumu hapa.
Karibu kwa comments hapa chini