Stori yake imenipa funzo, sitasahau!
Ilikuwa ni tarehe moja ya mwezi mwaka huu, mida ya saa saba mchana nilipokea ujumbe kwenye WhatsApp yangu kutoka kwa ndugu mmoja. Ujumbe huo ulisomeka hivi;
“Hellow mkuu habari, pole na majukumu, Nimesoma vitabu vyako viwili vya Uandishi wa kitabu kinachouzika na Kutoka kuandika mpaka kiiza kitabu,Vitabu vyote viwili vimenisaidia kunijengea msingi wa maarifa wa kunitoa kwenye mkwamo wa kuwa mwandishi mzuri wa vitabu”
Baada ya dakika chache, uliingia ujumbe mwingine kutoka kwa ndugu yule yule, ukiendelea kusema;
“Nakushukuru kwa maarifa haya Sasa nimeamua kuanzia kuchukua hatua kwa vitendo. Ninachokitabu cha kwanza ambacho ninaomba msaada wako wa kukifanya kuwa kitabu; Cover design, Kukihariri pamoja na kwamba tayari kimehaririwa kwa sehemu, na kupangwaversion zote za hard copy na Ile ya softcopy”
Nilitulia kidogo nikitafakari naanzaje kumjibu. Baadaye nilimjibu na ukawa mwanzo wa kufanya kazi na Gilbert. Sasa ameandika kitabu kizuri sana kinaitwa Hatari na Harasa za Kurudi Nyuma na Kuacha Wokovu.
Sasa nije kwako,
Pengine unajiuliza hivi ndo vitabu gani ambavyo Gilbert amesoma na vimempa mafanikio makubwa mno?.
Vitabu hivyo ni hivi hapa;
1. Uandishi wa kitabu kinachouzika. Unapoanza kusoma kitabu hiki unakuwa umeanza safari ya siku 25 za kuwa mwandishi aliyefanikiwa. Utafanikiwa kutimiza ndoto yako ya kuandika, na kuuza kitabu chako kwa mafanikio. Kwenye hatua yoyote uliyoko sasa kitabu hiki kitakuwa msaada kwako. Upo tayari kuanza siku 25 za kuwa mwandishi?
2. Kutoka Kuandika Mpaka Kuuza Kitabu. Unapokisoma kitabu hiki, utapata utajiri wa mbinu za kukusaidia kwenye kuandika, kutoa na kuuza kitabu chako. Pia utafahamu makosa ya kuepuka na namna ya kutatua makosa ambayo waandishi huwa wanakwama kupata utatuzi wake. Upo tayari kuanza safari nzito ya kusoma sura sita zilizoshiba?
Wengine waliosoma vitabu hivi ni Martin T, huyu alisoma kitabu cha Kutoka Kuandika Mpaka Kuuza kitabu na anasema kwamba, “Nimejifunza mengi kwenye kitabu hiki hasa aina za waandishi , taratibu za uchapaji wa kitabu, aina za uhandishi na kujua ukiandika kurasa ngapi za A4 utakuwa tayari umeandika kitabu chako hivyo Namshukuru Mwandishi wa Kitabu hiki kuna vitu vingi sana ambavyo nimejifunza toka kwenye uandishi wa kitabu hiki”
Kuna jamaa anaitwa Ozbon Kabembo, huyu yeye alisoma kitabu cha Uandishi wa Kitabu Kinachozika. Kwa furaha kabisa anasema kwamba, “Nichukue fursa hii kukushukuru, kwa elimu nzuri uliyotoa katika kitabu chako cha Uandishi wa kitabu kinachouzika. Hakika nimepata maarifa haya katika muda sahihi, nikiwa mbioni kumalizia uandishi wa kitabu changu, baada ya kusoma kitabu hiki nimegundua kuna mambo mengi sikuyafahamu ili kuwa mwandishi bora”
Chapisho hili limetolewa kwenye blog ya DaudiPages
Karibu kwa maoni hapa chini