Funguo 7 za mafanikio kwa Mkristo
Katika kujifunza habari za mafanikio kutoka kwa waandishi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi yetu nimekuja kugundua kwamba wengi wao wanachokisema ni sahihi lakini hakiwezi kumsaidia kila mtu.
Mara nyingi njia wanazozipendekeza haziweki bayana juu ya ni aina ipi ya mafanikio inayoweza kufikiwa kupitia njia hizo. Nje na aina ipi ya mafanikio inayopaswa kufikiwa, lakini bado njia hizo hazibainishi juu ya mtu yupi zinayemfaa hii ni kwa sababu hakuna mafanikio yasiyo na misingi na vilevile hakuna misingi inayohusu mafanikio isiyoambatana na sababu, malengo au matarajio kutoka kwa aliyefanikiwa kupitia misingi husika.
Vilevile ni muhimu ikumbukwe kuwa kuna aina nyingi sana za mafanikio na ni ngumu sana kuzitaja zote lakini kwenye kipengele kijacho tutakapokuwa tunaangazia maana ya mafanikio bila shaka nitaweka bayana baadhi ya aina za mafanikio.
Siku zote mafanikio ya hatua fulani yanategemea mafanikio ya hatua iliyotangulia na kila hatua ina Ufunguo wake ndiyo maana kwenye mafanikio huhitaji ufunguo mmoja bali Funguo Kadhaa na ndani ya kitabu hiki tutaangazia funguo muhimu saba. Mpaka hapo utakuwa umeelewa kwanini somo letu ni “Funguo Saba za Mafanikio kwa Mkristo” na siyo “Ufunguo wa Mafanikio kwa Mkristo”.