Kukaa kwenye nafasi yako
Mwanzo 3:9, “Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?”
Mungu anapouliza Adamu "uko wapi" haimaanishi alikuwa hajui walipojificha. Isipokuwa hakumuona Adamu kwenye nafasi aliyokuwa amemuweka. Ni nafasi ambayo Mungu alikuwa anakutana nao kila alipowatembelea. Kama kawaida, Mungu alipowatembelea awamu hii hakwenda mahali walipojificha bali mahali alipokuwa amewaweka. Hawakuwa nje ya Edeni, ila nje ya nafasi waliyowekwa na Mungu wakiwa ndani ya Edeni. Kwa hiyo unaweza kuwa hai lakini upo nje ya nafasi.
Nafasi ni nini basi? Nafasi ni mahali ambapo Mungu humuweka mtu ili aweze kumfanikisha kwa mafanikio ya rohoni na mwilini. Ni mahali ambapo Mungu akitaka kukutana na wewe anakuja hapo. Mtu anapokuwa nje ya nafasi ni wazi kuwa anapishana na mambo mengi sana ambayo Mungu anakuwa ameyakusudia katika wakati husika. Hakuna kilicho bora kutoka kwa Mungu kinachoweza kuendelea katika maisha ya mwanadamu akiwa nje ya nafasi.
Kuna tofauti ya kuitwa jina la nafasi na kukaa kwenye nafasi. Kuitwa jina la nafasi haina tofauti na kuitwa jina la cheo. Sio kila mwenye cheo basi anakitendea haki cheo husika. Umewahi kusikia watu wanasema pengo lake halitazibika? Au wanaposema bado hajapatikana mtu anayeweza kuvaa viatu vyake? Wanachojaribu kuzungumza ni suala la kukaa kwenye nafasi ipasavyo. Nchi inaweza kuwa na kiongozi mkuu wa nchi (Rais) lakini bado raia wakapata shida ambazo zinatakiwa kutatuliwa na Rais. Hapo nchi inakuwa na Rais jina tu. Hatima ya kiongozi kuendelea kuwa kiongozi imefichwa kwenye kukaa kwenye nafasi.
Ukicheza na nafasi uliyopewa na Mungu ujue wazi ni Mungu mwenyewe ndiye atakayekuondoa kwenye nafasi. Sasa unaitunzaje nafasi? JIPATIE KITABU.
Recommended for you

