Lishinde Jaribu
Jaribu lako ni nini? Ni kuachwa na mume au mke, kukosa watoto, kutokuolewa, elimu, cheo, changamoto za kazi au mahusiano, watu hawakuelewi, au hujui? Je, unapitia maumivu makali na mateso makubwa kwa sababu ya majaribu? Je, pamoja na vitu vyote vya ndoto yako unavyomiliki bado huoni raha ya maisha? Tumaini la kuendelea kuishi limepotea? Usijinyonge wala usikate tamaa!
Unawezaje kushinda hayo yote? Usichokijua ni kuwa bila ya kujali ukubwa wa jaribu na mateso yake, unaweza kushinda, kuendelea mbele na kusahau kabisa kama uliwahi kupitia hali hiyo. Geuza jaribu unalolipitia kuwa chachu ya kukupeleka katika kilele cha mafanikio yako.
Kitabu hiki kitakupa ufahamu kuwa; hali unayoipitia ni jaribu au mtihani. Pia, kitakupa mbinu rahisi za kushinda jaribu hata kama ni kubwa kiasi gani.