Maombi Ni Maisha Na Maisha Ni Madhabahu Ya Maombi
Maombi ni tendo la kiibada linalofafanuliwa kwa namna nyingi na kwa namna tofauti tofauti na watu mbalimbali, Maombi ndilo tendo la kiibada linalofanyika na jamii nyingi zaidi za kiimani Ulimwenguni. Maombi ndilo tendo na dhana iliyoelezewa kiutendaji mkubwa na kudhihilisha matukio makubwa ya kiimani Ulimwenguni. Katika ukinzani mpana wa nguvu zinazoaminika katika ulimwengu wa kiimani na imani zote, Maombi hufanyika kwa pande zote zenye ukinzani.
Tafiti zinaonesha kuwa imani zinazokua kwa kasi duniani na kubwa ulimwenguni kama Uislamu, Ukristu na Ubudha; licha ya utofauti mkubwa sana uliopo wa imani hizi katika misingi ya vitabu viaminiwavyo na Liturujia pana za dini hizi lakini “Maombi” hufanywa na imani zote zinazotajwa zikiwasilishwa kwa namna tofauti tofauti,utajo tofauti tofauti na hata Istilahi tofauti tofauti,kama vile sala, Dua, Maombi, Maombezi na Mazungumzo kwa aliye na uwezo wa vyote na hata Matambiko kwa miungu. Hii ni hoja ya msingi inayopaswa kutusaidia kung’amua kuwa Maombi si tendo la ibada tu, si tendo la kidini tu, Si utambulisho wa imani fulani tu, Si itikadi au ufanyaji kazi wa shughuli za kidini bali ni zaidi ya dini, Itikadi na Litulujia za kidini. Maombi ni zaidi ya Dini, Imani au Ufuasi wa kundi fulani la kiimani.
Hivyo Maombi ni nini basi? Nakukaribisha katika kurasa chache za kupitia siri hii iliyo njema na tamu sana itakapotambulika katika umaanani wake. Yaani MAOMBI. Nami Meshack ninayoshauku kubwa kuwa utakuwa na wakati wenye furaha zaidi unapotafakari dhana hii ya msingi sana, Nami sina budi kukualika ili tutambue kuwa.
MARANATHA! YESU ANAKUJA; MAOMBI NI MAISHA NA MAISHA NI MADHABAHU YA MAOMBI.