Moyo wa utoaji
MOYO WA UTOAJI: Ni kitabu kinacho elezea siri iliyopo tunapomtolea Mungu kwa Moyo wa kupenda bila kushurutishwa na mtu au mazingira. Sisi ni mawakili wa mali za Mungu. Vile tunavyotoa si mali yetu wenyewe. Bali tunamrudishia Baba sehemu ya mali yake aliyotupa kama dhamana. Kwani Mungu ndiye mmiliki wa vitu vyote. "Nchi ni mali ya BWANA pamoja na vyote vilivyomo ndani yake, dunia na wote wakao ndani yake" (Zaburi 24:1).
Amua leo kuwa mtoaji, lakini kumbuka kutoa kwa dhamiri safi mbele za Mungu. Hatutoi ili tuonekane na kusifiwa na watu. Tunatoa kwa Baba yetu wa mbinguni. "Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani ili watukuzwe na watu" (Mathayo6:2). Kumbuka kuwa si wingi wa sadaka unayotoa ndio yenye thamani mbele za Mungu bali ni moyo na thamani uliyokipa kitu kile unachokitoa. Utoaji si kwa matajiri tu, bali ni kwa watu wote. Pia utoaji si kwa washirika tu, bali utoaji ni kwa kila mtu tena viongozi tunatakiwa tuwe mfano bora wa kuigwa katika kumtolea Mungu. Kamwe usitoe sadaka huku unanung'unika au unatoa kama wajibu wako tu! Bali toa kwa moyo wa kupenda ukiwezeshwa na neema ya Mungu. Mungu anapenda mtu anayetoa kwa ukunjufu wa moyo na mtu anayesukumwa na upendo wake kwa Mungu.
Kumtolea Mungu
ni wajibu wenye Baraka, lakini wengi hawajui, hawataki au wazito kutoa.
"Moyo wa Utoaji" ni fundisho sahihi ambalo Mchungaji Nengala
ametuandikia. Soma ujue likupasalo, utende na ubarikiwe.