My Life is a Gospel (Maisha yangu ni Injili)
Kupitia kitabu hiki mwandishi ameonyesha jinsi alivyo na ujasiri mkubwa kutangaza habari njema za ufalme wa Mungu kupitia Maarifa mbalimbali kupitia vitabu vyake na kwenye mitandao ya kijamii na kuweza kufanikisha kuwasaidia watu wengi kumjua Mungu na wengi wametoa shuhuda za kumtukuza Mungu jinsi wanavyosaidika na maarifa yake.
Kama ambavyo neno la Mungu linatuonyesha jinsi ambavyo kazi ya kutangaza injili inahitaji ujasiri ndivyo ambavyo mwandishi ameamua kuishi kwa utayari na ujasiri kutangaza habari zinazoujenga ufalme wa Mungu.
Ukweli ni kwamba kupitia maarifa ya mwandishi watu wengi wanapata habari njema ya ukombozi wa fikra zao na roho zao kutoka gizani hadi nuruni na anafanya hayo kwa utayari na ujasiri kutoka kwa Mungu. Na shauku kubwa ya mwandishi ni kumfanya kila mtu aishi maisha ya ushuhuda na kudhihirisha tabia ya kuwa wakili mwaminifu wa Siri za Mungu kwa kila wakati.
1 Wakorintho 4:1-2 “Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu”
Kupitia maarifa ya kitabu hiki utapata mwongozo thabiti wa kuanza kuwa na maisha ya ushuhuda na wakili mwaminifu wa siri za Mungu. Kitabu hiki kitakukumbusha mambo muhimu kama:-
- Kumfanya Mungu awe dereva mkuu wa maisha yako ya kila siku.
- Kujikita katika mafundisho yanayosambaza ajenda za kuujenga Ufalme wa Mungu
- Kuzingatia neno la Mungu na maombi katika kuwafundisha na kuwaombea watu wengine.
- Kuwa na imani yenye matendo kwa kuyaishi maagizo na maelekezo ya Mungu kupitia neno lake na kutendea kazi maarifa haya kwa kuanza kuishi kuwa na maisha ambayo ni injili kwa wengine.
Chukua hatua sasa kww kusoma hiki kitabu na wewe kwa uaminifu zingatia huu mwongozo yafanye maisha yako na kila unachokifanya kuwa na ushuhuda na uwakili wa kumtukuza Mungu kwa waamini na wasio waamini.