Pasaka Wetu
Kumekuwa na Sikukuu nyingi za kuadhimisha kumbukumbu mbalimbali duniani kila mwaka. Kila taifa duniani huwa na siku yake maalum ya kukumbuka uhuru wake, ama tukio lolote muhimu katika historia yake.
Vivyo hivyo, Mungu naye ameteua siku yake maalum, siku ambayo aliamuru dunia nzima isherehekee na kufurahia uhuru na ukombozi wa mwanadamu. Siku hii si nyingine bali ni Siku ya Pasaka.
Pasaka ni nafsi. Pasaka ni uhai. Pasaka ni mateso ya mmoja kwa ajili ya ukombozi wa mwingine.
Katika Kutoka 12:21 tunasoma:
Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo, mkamchinje pasaka.
Isaka naye alikuwa na Pasaka wake.
Mwanzo 22:13 inasema:
Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
Wayahudi nao walikuwa na Pasaka yao.
Tunasoma katika Yohana 2:13:
Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.
Na sisi, kama ulimwengu mzima, tunaye Pasaka Wetu.
1 Wakorintho 5:7 inatufundisha:
Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo.
Recommended for you

