Tafsiri za ndoto
Je, unaandamwa na ndoto zinazokutisha au kukutatanisha kwasababu huelewi zinamaanisha nini?
Watu wengi hukumbwa na mabalaa au kupoteza fursa muhimu kwasababu waliota ndoto ambazo ziliwatahadharisha, kuwaonya au kuwapa mwongozo lakini hawakuchukua hatua yoyote kwasababu hawakuelewa ndoto hizo zilikuwa zinawambia nini. Hii ndiyo sababu imani na dini zote ulimwenguni zinautambua umuhimu na nguvu ya ndoto. Mfano mmoja mzuri unapatikana kwenye kitabu cha Mwanzo 41:1 ndani ya Biblia Takatifu na Surah Yusuf 12:43 ndani ya Kuran Tukufu. Nini kingetokea kama Yusufu asingetoa tafsiri ya ndoto zile?
Ndoto zako zinaweza kukwambia ikiwa maisha yako, kazi yako, mahusiano yako, afya yako au hata familia na wapendwa wako, viko hatarini. Kuna ndoto huwa ni maonyo na nyingine ni miongozo; zinakwambia usifanye hiki - pana hatari hapa, au fanya hiki - ndiyo njia yako ya mafanikio. Lakini kama hujui jinsi ya kutafsiri ndoto, ni dhahiri hutofanya chochote na utakumbwa na balaa au utapoteza fursa adhimu.
Ndani ya Kitabu hiki, Dkt. Dyaboli akishirikiana na Mchungaji Abel Muthembi, Sheikh Umar Al-Majid na Mganga wa Jadi Snubi wa Mandembo wanakufundisha jinsi ya kuzitafsiri ndoto unazoota ili uweze kuzitumia kama mwongozo wa mafanikio ya maisha yako.