Ukuaji wa Kiroho
Siku zote maisha ya kiroho yapo katika mwendo na sio katika kusimama na kutulia. Ni ama tunakua na kuongezeka kiroho au tunarudi nyuma na kufa kiroho. Kukua kiroho ni kwa msingi kwa kila mwamini, kama vile kukua kimwili kulivyo kwa msingi kwa maisha ya mtu yeyote. Kukua na kukomaa kiroho ni kwa muhimu sana kwasababu kupitia huko ndipo tunaweza kupata badiliko katika mwenendo wetu.
Katika kitabu hiki utapata fursa ya kujifunza mambo mengi ya msingi kuhusu ukuaji na ukomavu wa maisha ya kiroho kama vile:
- MAANA YA KUKUA KIROHO....
- UKUAJI WA MAISHA YA KIROHO...
- MCHAKATO WA UKUAJI WA KIROHO
- VIWANGO MBALI MBALI VYA UKUAJI WA KIROHO
- ALAMA ZA KUKUA NA KUKOMAA KIROHO
- KANUNI ZA UKUAJI WA KIROHO
"Nguvu nyuma ya kukua kwetu kiroho ni Roho Mtakati- fu. Yeye ndiye anatutia nguvu kukua kwetu; Anatupa uzima na uzima ni kukua".