Malipo ya Dhambi
LILA - mstaarabu na mwenye roho ya imani na anaamini haraka sana, anajali na pia ana moyo wa kusaidia na kutoa, anamuamini mno rafiki yake Salu na kutamani kumsaidia kimaisha.
SALU - mjanja wa mjini mwenye akili za haraka za kupata kipato kikubwa bila ya kufanya kazi. Anapenda pia maisha ya juu na hajali njia anayotumia kupata hicho kipato. Ni mzuri kwa sura na anapendeza, anawavutia wanawake wa aina zote na anawapata kirahisi huku moyoni akiwa na mipango yake tofauti na ya mapenzi.
MARIAM - uzuri wake unamfanya kila mwanaume atamani kua nae kimapenzi. Kuna muda alitaka kuolewa kwao Morogoro lakini fumanizi likavuruga mipango ya harusi yake akaamua kukimbia kabisa mji na kuhamia Mbeya.
Lakini jinamizi la hilo fumanizi halikumuacha, alikutana na na Lila ambae haraka sana akampenda na kumuoa hivyo akasahau kabisa alilokimbia Morogoro. Lakini Salu rafiki wa mumewe alijua siri zake za nyuma na kumtisha kwamba atazitoa kwa dada wa mumewe ambae toka mwanzo hakumkubali Mariam awe mke wa kaka yake ingawa hakua na uwezo wa kuizuia ndoa. Salu alitaka jambo gumu kwa Mariam na iwapo hatakubali matakwa yake nae atatoa siri zake zote anazozifahamu na kuharibu ndoa yake. Matakwa gani hayo? Mariam atakubali kuyatimiza hayo matakwa ili kuilinda ndoa yake?
Mwisho kuna Abraham, tajiri ambae ana roho mbaya na hajawahi kuchezewa wala kudhulumiwa na mtu, sifa yake kubwa ni kuua wanaotaka kumfanya mjinga, Salu kwa tamaa zake anaingia bila ya kujua katika anga za Abraham... Atasalimika?