Sentafowadi
Mwanana Chake Mutwa ni mwandishi wa habari kwenye gazeti la NIA, lililo na makao makuu kisiwani Zanzibar. Wadhifa na mkataba wa kazi unampa upeo wa kupachikwa jina la ‘Sentafowadi’. Mwanana hana budi kuishi maisha sambamba na maudhui ya wimbo wa taifa, “Mungu ibariki Afrika” kwani huripoti matukio ya kizalendo kila pande za Afrika.
Bi. Maimuna ni daktari wa moyo katika hospitali ya Muhimbili ambapo amegundua ugonjwa wa UMCUM (Ukosefu wa Maelezo kwenye chembe unaoshinikiza moyo). Ugonjwa wa UMCUM unaoambukiza unasambaa kila kukicha huku kusababisha watu kupooza na hatimaye kutupa mikono. Bi. Maimuna anamdokeza Mwanana na kumtahadhalisha kwani mkurugenzi wake bwana Fwedha ni ndumilakuwili na tajiri anaebania tiba ya UMCUM kwani anatumia kwa manufaa yake.
Je Maimuna na Mwanana watafaulu kusaidia jamii huku namna ya kuepuka na bwana Fwedha ni mtihani usio na kifani? Je kwa awamu hii jamii itajifunza nini na majanga kama UMCUM yanayo shinikiza mwili?