Wasomi Wajinga
Wasomi Wajinga ni tamthiliya ya kisiasa inayoangazia changamoto zinazokikumba kijiji cha Nyinyoro (nchi huru ya kiafrika) na jinsi viongozi wake wanavyotumika kama vibaraka wa Watu wa Chaki (Wazungu). Inajaribu kufichua nani ni nani, kwanini mambo yanakwenda yanavyokwenda, na kuangalia uwezekano wa kukikomboa kijiji toka kwenye meno ya Wanyinyoro walafi na Watu wa Chaki. Mmoja wa wanakijiji anasema ‘Kwakweli hali ni tete; majalalani sasa mbwa na paka wanakula hadi viatu! Nani wa kutupa ugali? Kila kitu kimepanda bei isipokuwa pombe, sigara na kondom. Sura za watu zimezidi kuwa mbaya maradufu. Wanaume watapata wapi nguvu za kiume na hali ya maisha ilivyo?’ Vilio vimetapakaa. Wanaikumbuka kauli-mbiu ya kiongozi aliyepita:
‘Usipojikaza Unakazwa!’