Kijana wa Mfano - Kanuni kuu saba za kijana wa mfano
Kila kijana anatamani kuona maisha yake kuwa bora kabla hajaingia katika majukumu ya kifamilia, ndoa au kuvuka umri na kwenda utu uzima. Ila wengi husahau kanuni za kufika kule wanapotaka hivyo hujikuta wakiishi maisha ya kawaida sana na wao kuwa wa kawaida yaani hakuna matokeo na ndio hali ya vijana wengi katika maisha ya leo. Ukweli ni kwamba, “Hakuna maisha mapya na ujana wa mfano wenye
thamani na ubora pasipo mtu mpya mwenye mtazamo mpya na ulio chanya Wengi wanaishi katika maisha wasiyo yataka ila kutokana na kutojua kanuni au kujua na kutozingatia ili kuwa kijana wa mfano hubaki vile vile tu na maumivu ya kutofikia ubora wanaotaka kufikia. Maisha ya hapa duniani katika jambo lolote kuna kanuni zake. Kwa wale wanaozingatia hizo kanuni ndio hufanikiwa lakini ukizivunja kanuni maisha yako yanakuwa hatarini kwenye kuelekea anguko lako.
Mfano kanuni ya kuwa na uzee mwema inakutaka ujitume ukiwa kijana ili usijute uzeeni na hakikisha katika jambo lolote unalofanya kuhudumia jamii unalifanya katika ubora ili uwe wa mfano kwa wengine na huduma kama yako ikihitajika mtu wa kwanza kutajwa uwe wewe. Kanuni hizi hazina uhusiano kabisa na mtu ambae atasoma na kuziacha kama zilivyo. Lakini zina mahusiano na mtu ambaye atasoma kwa umakini na utulivu mkubwa halafu akaingia kuwa mtendaji. Yaani kuwa mtu wa vitendo na huyu ndiye atakayeona mabadiliko chanya katika maisha yake na kuwa kijana wa mfano.
“Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio , katika usemi na mwenendo nakatika upendo na Imani na usafi” (1 Timotheo 4:12)
Naona ukianza kuwa kielelezo na bora zaidi nakuwa mkuu kama utachukua hatua kuzingatia kanuni hizi unakuwa mfano halisi kwa vijana wengi. Jambo la msingi sana kwa kila kijana anayefanya shughuli au huduma yoyote kufanya mambo yake kwa mfano halisi ili wengine wajifunze kupitia yeye afanyavyo. Pia inabidi afanyike sehemu ya kuwatengeneza vijana wengine wanaofanya mambo yao katika ukawaida bali kupitia yeye wafanye kwa ubora na thamani zaidi. Jambo la muhimu ni kutoa huduma au bidhaa bora ili popote inapohitajika mtu wa kwanza kutajwa uwe wewe.
BAADHI YA KANUNI ZA KUZINGATIA KUPITIA KITABU HIKI:-
- Kanuni ya Imani.
- Kanuni ya kujitambua
- Kijana na maono na malengo
- Kanuni ya uwajibikaji na kufanya kazi
- Kanuni ya elimu, maarifa na malezi sahihi.
- Kijana na Saikolojia
- Kanuni ya Kujitathimini.
JITATHIMINI HALI YAKO YA KUZINGATIA MAARIFA, WEWE NI KIJANA WA MFANO.
“Ujinga ni kufanya jambo moja mara kwa mara kwa namna ileile na kutegemea matokeo ya aina tofauti’’ (Albert Einstein)
Kujitathimini, hii ni hatua ya kipekee sana na kishujaa anajifanyia kijana mwenye upendo wa kweli na maisha yake ili kujichunguza maisha yake binafsi katika hatua binafsi kuanzia alipotoka, alipo na anapokwenda.
KILA MTU ANAFANYA UNACHOFANYA, KINACHOTAKIWA UJUE KANUNI ZA KUFANYA KWA UBORA NA UTOFAUTI. KUWA KIJANA WA MFANO INAWEZEKANA.