Kiongozi Aliyechoka
Tunaishi katika ulimwengu uliojaa viongozi waliochoka, mfumo wa maisha umepelekea kuwa na viongozi wa namna hii, na wengi hufa mapema kwa sababu ya kuchoka. Kutokana na shinikizo la maisha na kutaka kufanikiwa viongozi wengi huteketeza na kupoteza nguvu zao kwa kasi. Majukumu ya kihuduma wanayofanya kila siku yananyonya na kuteketeza nguvu zao (kimwili, kihisia, kiakili na kiroho) na kama hawana maarifa ya kuzirejeza watajikuta kwenye hali ya uchovu kisha kuteketea kabisa kwa nguvu. Hali hii itaathiri afya zao, akili zao, hisia na roho zao pia.
Kila kiongozi anapaswa kujilinda na hali hii kwa kujua dalili za uchovu na tiba yake, na nini afanye kuzijereza nguvu zake pale zinapoteketea. Katika kitabu hiki utapata fursa ya kujifunza mambo muhimu ya kukusaidia na kukuongezea maarifa na ufahamu juu ya eneo hili muhimu.