Kutoka kuandika mpaka kuuza kitabu
Ilikuwa ni kiu yangu ya muda mrefu kuandika kitabu kimoja ambacho mtu akikisoma atakuwa amepata vitu muhimu sana na vya msingi kwenye uandishi wa vitabu kuanzia hatua ya kuandika mpaka kuuza kitabu.
Kwenye kitabu hiki nimeshughulika na mambo matatu;
- Ufahamu wa mbinu za kukusaidia kuandika, kutoa na kuuza kitabu chako. Uandikaje kitabu? Mchakato wa kutoa kitabu ukoje? Kitabu kinafikaje kwa wasomaji na unakiuzaje?. Unapokisoma kitabu hiki, utapata utajiri wa mbinu za kukusaidia kwenye maeneo yote haya
- Ufahamu wa makosa ya kuepuka. Huwezi kuepuka kosa usilolijua, hivyo nimeanza kwa kukuonesha makosa yenyewe ili uweze kuyaepuka.Kuyaepuka makosa haya itakusaidia kuufurahia uandishi wa vitabu kwa kuyachuma mafanikio yake.
- Kutatua makosa ambayo waandishi huwa wanakwama kupata utatuzi wake. Makosa haya hujitokeza kuanzia hatua ya kuandika mpaka kuuza kitabu. Kusoma kitabu hiki kutakupa kujua jinsi ya kutatua makosa hayo.
Huishii tu kusoma kitabu. Upo huru kabisa kupata usaidizi kutoka kwangu, unapoendelea kusoma kitabu na ukaona kukwama kwenye jambo fulani, wewe nitumie meseji au nipigie, tutazungumza!
Upo tayari kuanza safari nzito ya kusoma sura sita zilizoshiba? Haya anza!
Recommended for you
Customer reviews
★★★★★
MARTIN T., 13 Jan, 2024
Nimejifunza mengi kwenye kitabu hiki hasa aina za waandishi , taratibu za uchapaji wa kitabu, aina za uhandishi na kujua ukiandika kurasa ngapi za A4 utakuwa tayari umeandika kitabu chako hivyo Namshukuru Mwandishi wa Kitabu hiki kuna vitu vingi sana ambavyo nimejifunza toka kwenye uandishi wa kitabu hiki.