MWAKA MPYA
Kila mtu anapouanza mwaka mpya huwa na ndoto, mipango na malengo makubwa anayopenda kuyatimiza. Lakini kwanini wengi huanza na moto mkali halafu huishia njiani? Kwanini baadhi wanafanikiwa na wengine wanakwama kila mwaka?
Katika kitabu hiki, Abel J. Ngeleja anakupa mwongozo wa vitendo – mambo 10 muhimu unayopaswa kuyafanya ili malengo yako ya mwaka huu yaweze kutimia kwa mafanikio makubwa.
Utafundishwa:
- Umuhimu wa kuandika malengo yako
- Jinsi ya kupanga mipango yenye mafanikio
- Hatua za kushinda vikwazo vinavyoweza kukuzuia
- Mbinu za kujenga nidhamu binafsi
- Mikakati ya kujipima na kujirekebisha
- Njia za kushirikiana na watu sahihi katika safari yako
- Na mambo mengine ya msingi kwa mafanikio yako
MWAKA MPYA si tu kitabu cha kusoma — ni ramani ya maisha yako kwa mwaka mzima. Ni kama kifurushi cha nguvu (package) kilichojaa kanuni, tafiti, ushuhuda na mbinu madhubuti zitakazokusaidia kuacha kuishi kwa mazoea na kuanza kuishi kwa ushindi.
Unapopambana na kupigania mafanikio yako kwa nguvu sawa na ulivyopigania pumzi ndani ya maji – utashinda.