Nguvu ya Kujifunza kupitia Semina na Mafunzo mbalimbali
Kujifunza ni jambo muhimu kwani linasaidia kukupa mwanga katika maisha yako.
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kwamba watu walio katika hatari kubwa ni ambao wanadhani wanajua kila kitu. Tabia hii ni mbaya kwani huzuia maendeleo.
Unapoacha kujifunza unazuia maendeleo yako na maendeleo ya jamii kwa ujumla. Jifunze ili upige hatua moja kuelekea ndoto ya maisha yako.