Uandishi wa kitabu kinachouzika
Mwenye ndoto ya kuandika na kutoa kitabu ni wewe si mtu mwingine, mwenye ndoto ya kuuza nakala nyingi ni wewe na si mtu mwingine, na mwenye ndoto ya kuwa mwandishi aliyefanikiwa ni wewe na si mtu mwingine. Kwenye hatua yoyote uliyoko sasa; iwe kuandika, kutoa ama kuuza kitabu chako, kitabu hiki kitakuwa msaada kwako.
Unapoanza kusoma kitabu hiki unakuwa umeanza safari ya siku 25 za kuwa mwandishi aliyefanikiwa bila stress. Utafanikiwa kutimiza ndoto yako ya kuandika, kutoa na kuuza kitabu chako kwa mafanikio.
Msukumo wangu wa kuandika kitabu hiki ni kukushirikisha uzoefu wangu kwenye uandishi wa vitabu utakaokusaidia wewe usikwame kwenye kutimiza ndoto yako. Nimeunganisha uzoefu wangu wa kuandaa kozi za uandishi, niliyopitia kwenye kutoa vitabu vyangu na ushauri niliotoa kwa watu mbalimbali waliokuwa wamekwama hatua walizokuwa kwenye uandishi wa vitabu.
Kwa kifupi, kitabu hiki kinamfaa yeyote anayetaka;
- Kuandika kitabu
- Kutoa kitabu
- Kuuza kitabu
Ninaposema uandishi wa kitabu kinachouzika, naamanisha kuwa uandike kitabu kitakachofika mkononi mwa msomaji wako na hiyo ndiyo furaha ya mwandishi yaani kuona msomaji amesoma, amejifunza na kukifurahia kitabu.
Upo tayari kuanza siku 25 za kuwa mwandishi aliyefanikiwa? Upo tayari kuandika kitabu kitakachofika kwa msomaji wako?
Recommended for you
Customer reviews
★★★★☆
Neema, 20 Sep, 2023
Amazing book that I have ever read. Thanks Daudi for this masterpiece.