Vuka Ujana Salama Inawezekana
Nikupe uhakika wa kupata majibu ya maswali haya sita;
- Kwanini kuvuka ujana salama na sio tu kuvuka ujana?
- Tofauti ya mtu anayevuka tu ujana na anayevuka au aliyevuka ujana salama
- Kwanini inawezekana kuvuka salama na inawezekanaje?
- Kama kijana unawezaje kujitambua zaidi hadi kujua sababu halisi ya uwepo wako duniani yaani kusudi lako.
- Unawezaje kushinda mapambano dhidi ya maadui wakuu hawa, Umaskini , maradhi na Ujinga?
- Unawezaje kuongeza thamani na ubora zaidi wa maisha yako katika nyanja zote muhimu?
Kwa hakikaa hiki kitabu kinakupa maarifa sahihi ambayo ni mwongozo thabiti kwa maisha ya kijana yeyote anayetamani kuvuka salama katika ujana wake, huku akizidi kuuishi Ujana wenye matokeo mazuri na maana halisi yenye kuzidi kumjengea kesho yenye thamanina ubora zaidi.
Soma huku Ukikumbuka maneno ya Baba wa Taifa , Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere.Aliyetuachia mapambano dhidi ya maadui wakuu watatu wa kupambana nao kila siku kuwa ni “UMASKINI, MARADHI na UJINGA”.
Na wahusika wa muhimu sana na wenye nguvu na uwezo wa kuweza kuleta mageuzi na ushindi mkubwa katika mapambano dhidi ya hao maadui ni vijana.
Pambana na umaskini kwa nguvu zote; elimu ya fedha kwa wingi, maarifa sahihi, biashara, bidii katika shughuli za kiuchumi n.k na mhusika mkuu ni wewe kijana unayesoma. Pambana na maradhi, tunza afya yako ikutunze ,jali afya yako, acha kufanya vitu vinavyohatarisha afya yako, bado wewe ni wa thamani na unategemewa na familia, Jamii, nchi na dunia. Pambana na ujinga, jifunze kila siku, mwisho wa kujifunza sio baada ya kuhitimu masomo, Kujifunza ni kila siku, eneo fulani ambalo hauna maarifa ya kutosha linakuhitaji ujifunze zaidi ili ufanye kwa ubora zaidi.
Tuache mitazamo mibaya kwamba kuvuka ujana salama haiwezekani, acha kujidharau au kudharau ambao wanakushauri hata kama ni rika moja kama wamepata maarifa fulani wanapokusaidia nyenyekea kusikiliza.
Zaidi ya yotee amini kuwa kuvuka ujana salama inawezekana na hakikisha unaishangaza dunia kwa kuanza kuwa kijana wa matokea Chanya kuanzia sasa. Kumbuka maneno ya Hayati Raisi wa kwanza wa Afrika Kusini na mpiganaji wa Ukombozi wa taifa hili, NELSON MANDELA aliyasema katika uhai wake kuwa, “ It seems impossible , until it is done”. Akimaanisha kuwa inaonekana ni vigumu mpaka utakapofanikisha hiyo azma yako, hata kwake kufanikisha uhuru waTaifa laAfrika Kusini haikuwa rahisihata kidogojapo alifanikisha, hata kwako sio rahisi kuvuka salama lakini jipige kifuana jiambie kwa sauti kuwa INAWEZEKANA, kikubwa kujifunza na kuzingatia zaidi.
Zingatio muhimu "NI KOSA KUBWA KWA MWANADAMU KUIVUKA HATUA YA UJANA PASIPO KUACHA MATOKEO CHANYA”. Hakikisha unapata muda kutafakari kauli hiyo, kuwa maisha ya Ujana wako, yanaacha matokeo chanya au hasi kwa Jamii yako
NA KUPITIA KITABU HIKI UATAJENGA MTAZAMO CHANYA NA KUKUPA NGUVU NA HAMASA YA KUACHA MATOKEO CHANYA KWA JAMII.
Wewe ni wa muhimu sana katika kuleta matokeo chanya, hebu sema kwa sauti mara tatu, huku ukijipiga kifua kauli hii;“KUVUKA UJANA SALAMA INAWEZEKANA”.