Nuru ya Upendo
NURU YA UPENDO ni kitabu kimechojikita katika mahusiano ya kimapenzi ikiwemo uchumba na ndoa.
Nimejaribu kuyaangalia mahusiano katika jicho la tatu ili kuboresha, kuimarisha na kutatua matatizo na changamoto kwenye mahusiano pia namna sahihi ya kuishi ndani ya mahusiano.
Katika mahusiano kuna mambo makuu manne ambayo ni; kuimarisha mahusiano, kuboresha mahusiano, kutatua migogoro katika mahusiano na kuyalinda mahusiano. Kitabu hiki pekee kimeweza kugusa hizo nyanja zote.
"NURU YA UPENDO" jina hili linasadifu kilichomo ndani ya kitabu kwani wengi wapo kwenye mahusiano ambayo yako ndani ya giza, tunajua kuwa ukiwa kwenye giza huwezi kufanya mambo yako kwa weledi, hivyo kitabu hiki kinaweka nuru ya mwangaza kwa kukupa maarifa katika upendo.
Recommended for you
Nitaiambia nini familia yangu
TZS 10,000
Uchumba Kuelekea Ndoa Takatifu
TZS 3,000
SEXUS: Siri za Ngono Tamu