Tupo kwenye dunia iliyojawa na vurugu na watu wa kila namna, ukuaji wa teknolojia na suala zima la mitandao ya kijamii pamoja na kwamba ni vitu tunavyo vihitaji sana katika maisha ya sasa na ya baadae, lakini vitu hivi kwa kiasi fulani vinaonekana kuwa ni tishio kubwa kwa makuzi na malezi ya watoto. Watoto ni Taifa la kesho, ni hazina inayopaswa kulindwa na kutunzwa katika ubora na maadili mema kwa ajili ya kizazi na Taifa lijalo. Mzazi, mlezi, au mzazi mtarajiwa, usiache kupitia kurasa na sura zote za kitabu hiki, kuna mengi mazuri ya kukusaidia juu ya watoto wako. Maisha ya mtoto wako, yapo mikononi mwako, jifunze mbinu bora za kimalezi juu ya maisha ya mtoto/watoto wako.