Ichaji Akili Yako Ya Fedha
Pesa zinasikia, zinaona na zina hisia. Pesa Zina kawaida ya kuitana, ndio maana zikiwepo sehemu kuna uwezekano zikaendelea kuongezeka. Kinachoamua kiwango cha pesa anachoweza kumiliki mtu, sio kiwango cha kipato wala aina ya chanzo cha kipato bali ni akili ya fedha aliyonayo mtu husika.
Katika kila kazi kuna faida na utajiri. Kwa nini katika kazi ya aina moja wawepo wenye nazo na wasio nazo? Majibu ya swali hili yanapatikana katika kitabu hiki ambacho umalizapo kusoma utakutana na mguso wa mgeuko wa jumla katika eneo la fedha!