Mpenyo - Nidhamu ya fedha
Sentensi nitakayosema hapa huwa inawakasirisha watu wengi sana. Pengine inaweza kukukasirisha hata wewe pia! Matatizo yako ya Fedha hayasababishwi na Serikali, Uchumi, Bosi wako, Baba au Mama mwenye nyumba yako, Mchumba, Mume/Mke n.k, Amini usiamini matatizo uliyonayo yanasababishwa na wewe Mwenyewe!
Kutokana na
Mtaalam wa Masuala ya Fedha na Uwekezaji Ndugu Dave Ramsey, anatuambia kwamba
matatizo ya kifedha kwa Asilimia 80 yanasababishwa na tabia zako wakati
asilimia 20 yanasababishwa na kukosa maarifa sahihi. Hivyo ili kufanikiwa
kifedha, licha ya kujifunz na kujiongezea Maarifa ya kichwa ni lazima
kushughulikia Tabia zetu na kuzikabili, hii inamaanisha uwe tayari kuishi
tofauti na unavyoishi sasa.
Kama mtu ni
Mgonjwa, njia rahisi ya kupona kwanza ni kukubali kwamba anaumwa. Tatizo watu
wengi hawapendi kukubali kwamba wana Tatizo fulani. Hili huwafanya wasitafute
Usumbufu wa
matatizo yao. Uzoefu wangu unaonesha kuwa Wanaume wana tatizo hili zaidi kuliko
Wanawake, kama una matatizo ya Kifedha na umenuia kuyaondoa ninategemea sio tu
kwamba utakubali, bali ninategemea utafanya Juhudi kuangalia au kuelewa Ukubwa
wa tatizo ulilonalo. Ili kujua hali ya Afya yako ya kifedha na kama uliruka
zoezi Tathmini ya Afya yako ya Kifedha(Financial Intelligence Test) lililoko
Mwanzoni wa Kitabu hiki, huu sasa ni Wakati wa kurejea na kulifanya na kupata
Tathmini Halisi.