Uchumi na Kanisa la leo
Kitabu hiki cha ―UCHUMI NA KANISA LA LEO‖ kimeandaliwa maalumu kwa ajili ya kumsaidia mwamini kupata misingi itakayomwezesha kukua kiuchumi kwa kupitia kujua utimilifu wa ahadi za Mungu kwa mwanadamu juu ya uchumi kupitia kuteswa kwake kristo ― kwa kupigwa kwake sisi tumepona!
Kwa sababu ya ustawi kiroho na kimwili, kuna umuhimu mkubwa sana kwa mwamini kujifunza suala la uchumi. Mwanadamu ana mahitaji ambayo hayaishi na huwa yanakawaida ya kujirudia mara kwa mara kwa mfano mahitaji ya chakula, mavazi, mawasiliano, usafiri, matibabu na huduma za kila siku kama umeme, maji na kulipia gharama za elimu kwa watoto.
Kanisa linahitaji fedha
(uchumi imara) kwa ajili ya kuendeleza kazi ya kuujenga ufalme wa Mungu.
Waumini wa kanisa wanahitaji uchumi ili waweze kuhusika katika ujenzi wa kanisa
na kuchangia huduma mbalimbali ndani ya kanisa.
Waumini
wana mahitaji ya kila siku, mahitaji yanayowafanya wakati mwingine licha ya
kuwa na moyo mzuri, wanashindwa kushirika shughuli mbalimbali zinazogusa eneo
la uchumi Kama vile sadaka, fungu la kumi, michango ya ujenzi na maendeleo,
kuwatunza watumishi wao, kama wachungaji na walimu wao pamoja na kuanzisha
miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Dhima kuu katika kitabu hiki ni kuleta mabadiliko chanya kwa kanisa la leo na kumsaidia mkristo kujua misingi ya uchumi na ahadi za mungu kupitia biblia takatifu. Aidha kukuza ari ya kujitambua, kujithamini, kujiamini, kuthubutu na kuamua kuanza kuchukua juhudi za makusudi kufikia uchumi mkubwa.