Wewe na Pesa
Fedha kiungo muhimu cha kubadilishana bidhaa na huduma katika zama hizi inaonekana kutotosheleza mahitaji kila uchwao. Hali hii imepelekea watu wengi kulemewa na madeni yasiyolipika; je, nini kifanyike?
Kitabu hiki kimeandikwa kutafsiri changamoto mbalimbali za maisha zihusuzo masuala ya fedha. Mwandishi anakuletea mbinu mbalimbali ambazo unaweza kuzitumia ili fedha unazozipata sasa na zile utakazozipata katika siku za usoni ziweze kukusaidia kukabiliana na changamoto za maisha yako ya leo na kukuweka tayari kuikabili kesho ukiwa bora Zaidi kuliko jana na leo. Masuala kama madeni na tiba yake, chuma ulete?, kutimia kwa ndoto, siku muhimu katika maisha, napataje mtaji yamejadiliwa.
Mwandishi anakusudia kwa dhati kwamba kurasa za kitabu hiki ziguse maisha yako na kuyafanya kuwa bora Zaidi.
Recommended for you


