FALSAFA ZA JPM
Katika historia ya Tanzania, hayati Dkt. John Pombe Magufuli (JPM) alisimama kama kiongozi wa kipekee aliyekuwa na falsafa chanya, imani madhubuti na msimamo usiotetereka kwa manufaa ya taifa lake. Kitabu hiki kimekusanya na kufafanua kwa undani falsafa 10 muhimu zilizomfanya JPM kuwa kiongozi wa mfano na mzalendo wa kweli.
Kupitia uandishi wa Abel J. Ngeleja, msomaji ataguswa na mafundisho ya kipekee kuhusu:
- Umuhimu wa kumtegemea Mungu katika kila jambo
- Nguzo ya kuchapa kazi bila kuchoka
- Kutambua na kuthamini utajiri wa rasilimali za Tanzania
- Umoja na mshikamano wa Watanzania bila ubaguzi
- Uongozi kuwa ni dhamana kwa watu wote
- Mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi
- Umuhimu wa kukuza na kuenzi lugha ya Kiswahili
- Uhuru wa kweli kuwa ni uhuru wa kiuchumi
- Kuishi kwa kusema ukweli bila woga
- Uzalendo wa kweli – “Tanzania Kwanza”
FALSAFA ZA JPM si tu kumbukumbu ya maneno na vitendo vya kiongozi aliyepita, bali ni mwongozo wa kizazi cha sasa na vijavyo kujifunza, kufundishwa na kuendeleza yale mema aliyoyaamini na kuyasimamia kwa nguvu zote.
Ikiwa unahitaji maarifa ya uongozi, uzalendo, nidhamu ya kazi na utetezi wa wanyonge – basi kitabu hiki ni hazina isiyopaswa kukosekana kwako.