Upentekoste na Uamsho katika Siku za Mwisho
Upentekoste na Uamsho katika siku za mwisho ni kitabu kinacho jaribu kufunua siri ya Kanisa kuendelea kuwepo tangia lilipo anzishwa na Yesu kupitia umwagiko mkubwa wa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste richa ya upinzani mkubwa kutoka kwa shetani, pamoja na mateso mengi waliyopitia wafuasi wa Kristo katika miongo na karne nyingi, pia kitabu hiki kinaelezea hali ya mwanzo kabisa ya kanisa likiongozwa na Roho Mtakatifu na kusababisha mapinduzi makubwa ulimwenguni, kiasi kwamba waliomkiri Yesu Kristo waliitwa WAPINDUA ULIMWENGU, Lakini hali mbaya ya kanisa iliyopo sasa imesababisha Dunia kuingia Kanisani kiasi kwamba DUNIA INAPINDUA KANISA, Kanisa limepoteza nguvu na ushawishi kwa wenye dhambi. Sasa Roho Mtakatifu anachilia nguvu ya Uamsho na Urejesho katika siku hizi za mwisho kwa kila mwenye kiu, ili kuliandaa Kanisa na kurudi kwake mara ya pili, Kanisa lisilo na mawaa wala kunyanzi.
Dhumuni la kitabu hiki ni kuwandaa waamini kujua majira halisi ya nyakati za kanisa na hali mbaya inayolikumba Kanisa la sasa na kujiweka tayari ili waweze kupona na nyakati mbaya za kutisha na kuchukua jukumu kutaka tena nguvu ya Mungu ili kurejesha uhai mpya wa Kanisa kama Mungu alivyokusudia kanisa liwe na nguvu ili kuweza kuyashinda malango ya kuzimu na kutangaza ufalme wa Mungu duniani.
Mapendekezo kwa ajili yako
