Unaweza Kuwa Unayemtaka
Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Unayemtaka na Kupata Chochote Unachokitaka Kwenye Maisha Yako.
Je una kiu na shauku ya kuwa unayemtaka?
Je unataka na kutamani kuwa wewe, uliyekusudiwa kuwa katika maisha yako.
Je unataka na kutamani kufanya biashara au kazi ya ndoto yako, uliyokusudiwa kuifanya hapa duniani? Lakini hujui uanzie wapi?
Je unajiuliza utagunduaje kusudi lako, kipaji chako, wito wako na kuutumia hapa duniani ili kupata chochote unachotaka?
Je unafahamu ipo ndani ya uwezo wako kuwa unayemtaka, unaweza kuwa unachokitaka na kupata chochote unachotaka?
Na je ungependa kufahamu kanuni muhimu na miongozo ya uhakika ya kufuata ili kuwa unayemtaka, na kupata chochote unachotaka?
Kama umesema NDIYO kwenye swali lolote hapo juu, basi kuna HABARI NJEMA kabisa kwako hapa.
Habari njema ni kwamba, unao uwezo ndani yako wa kukufanya uwe unayemtaka na kupata kile unachokitaka. Kama usingekuwa na uwezo huo, usingetamani au hata tu kutaka kuwa unayemtaka, kwa sababu hakuna anayeweza kutamani na kuhitaji au kutaka kitu asichokijua au kutokukitaka.
Sasa leo unakwenda kujifunza ni kwa namna gani unaweza kutumia kanuni za kuwa unayemtaka na kupata chochote unachokitaka.
Kwenye kitabu kinachoitwa UNAWEZA KUWA UNAYEMTAKA, unapata nafasi ya kutambua uwezo mkubwa ulioko ndani yako, uko wapi, unaufikiaje na unawezaje kuutumia ili kuwa unayemtaka na kupata chochote unachotaka maishani mwako.
Baadhi ya yale unayokwenda kujifunza kwenye kitabu hiki ni;
Jinsi ya kutumia Imani na kuamini kwako, ili akili na ubongo wako ukuwezeshe kuwa unayemtaka, na kupata chochote unachokitaka. Akili yako na ubongo wako vina uwezo wa kufanya na kutafuta chochote kinachotakiwa na kuhitajika, ili wewe uwe unayemtaka, lakini kama tu utaamini kuwa unaweza kuwa unayemtaka
Jinsi nguvu ya kuamini inavyokuwezesha:
- KUWA; mafanikio yoyote lazima uwe. Kabla hujayapata mafanikio unayoyataka, hatua ya kwanza ni wewe kuwa. Kuanza kuishi maisha ya kile unachokitaka.
- KUFANYA; Nguvu ya kuamini, inakusaidia pia kuweza kufanya kile ambacho umekuwa.
- KUPATA; nguvu ya kuamini inakuwezesha kupata chochote unachokitaka.
Jinsi ya kuyaendesha maisha yako. Utajua umuhimu wa kushika hatamu ya maisha yako, kwani wewe ndiyo dereva wa maisha yako. Utaachana na kulalamika, kulaumu, kuhukumu lakini pia utafanya uchaguzi na maamuzi yaliyo bora wewe mwenyewe bila kusubiri mtu mwingine akufanyie.
Jinsi ambavyo unaweza kukua kila siku. Ndiyo, unatakiwa ukue kila siku kama kweli unataka kuwa unayemtaka, usiwe na ukomo wa matumizi. Utajifunza kwa kina nini cha kufanya kila siku ili uwe unachotaka na kupata kile unachotaka.