Deni la dhababu
Kitabu, “Deni la Dhahabu” ni kati ya
vitabu vichache sana sokoni ambavyo vinaweza kubadilisha namna
unavyofikiri kuhusu mali na hali yako halisi ya
kiuchumi. Chanzo cha umaskini au utajiri ni
jinsi mtu awazavyo, “Awazavyo/aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo” (Mithali 23:7). Kama ukiweza kuwaza sahihi
kuhusu jambo fulani, utalipata jambo hilo; Na, ukiwaza
vibaya kwa namna hasi, bila shaka utalikosa.
Mawazo ni vitu, tena vitu halisi; Kitabu hiki
kinakupa sio tu namna ya kufikiri lakini pia jinsi ya kufikiri.
Mwandishi wa Kitabu hiki, Gastor Hilary Mtweve, amejikita kwenye “falsafa ya uhalisia wa mambo” (Pragmatism), ambayo inamfanya msomaji aone uhalisia wa maisha yake mwenyewe na sio nadharia tu, au watu wengine wanavyo muona. Kila aliyefanikiwa kimaisha alifanya uamuzi wa dhati wa kukubali ukweli (kwamba hali ni mbaya), na akachukua hatua za kupambana na hali yake ili kujikwamua. Huu ni uamuzi wa mara moja lakini matokeo yake yanaweza kuja baada ya muda mrefu kulingana na mazingira ya mhusika.
Kitabu hiki ni kiongozi mzuri wa
kukuwezesha kuchukua hatua za
mabadiliko ya maisha yako hasa ya kiuchumi.