Jiandae Kustaafu
“Kujiandaa kustaafu huanza siku ya kuajiriwa, mtu ambaye amejiandaa vizuri ni yule ambaye ametambua kuwa kuna kustaafu tokea siku ya kwanza ya ajira. Kuna maandalizi ya kiuchumi, lazima mtu awe na ndoto ya kuwa akistaafu anataka kuishi maisha gani, atafuatilia kama michango yake inawasilishwa kwenye mfuko, ataweka mikakati ya kujiwekea akiba. Maandalizi ya kijamii. Je, ukistaafu unastaafia wapi? Kujiandaa kisaikolojia. Kustaafu ni kweli. Kustaafu ni halisi. Kustaafu kupo na kunatokea kweli. Maandalizi ya kiafya. Ni muhimu uanze kujipanga utastaafu vipi?” Victor A Kikoti, Meneja Matekelezo Mfuko wa PSSSF.
“Tafiti mbalimbali zimebaini kuwa wastaafu wengi hukumbwa na misukosuko mingi ya kifedha, kiafya na kimaisha kwa ujumla. Moja kati ya sababu kubwa ya wastaafu kukumbwa na misukosuko hiyo ni kushindwa kuhimili vyema na kutokuwa na mipango madhubuti ya maisha baada ya kustaafu kazi.” Tanzania Global Learning Agency
“Muda mzuri zaidi wa kujiandaa kustaafu vizuri ni siku unapoajiriwa kwa mara ya kwanza. Kiinua mgongo chako hakipaswi kuwa ni fedha ya kuandaa maisha baada ya kustaafu.” Hayati Profesa Honest Prosper Ngowi.