Msimu wa Ndoto - Tafsiri ya 'A MidSummer Night Dream'
Hadithi hii ni tafsiri ya mchezo wa William
Shakespeare ujulikanao kama 'A MidSummer Night Dream'. Mchezo huu una mbinu
tosha za kifasihi na matumizi mazuri ya lugha.Kazi ni ya tanu katika msururu wa
tafsiri hizi ambazo za awali ni Juliasi Kaizari na Mabepari wa Venesi (Julius
Nyerere); na Makbeth na Tufani (Samuel Mushi).
Kitabu hiki kitamfaa mwanafunzi wa Kiswahili katika kiwango chochote cha usomi
wake. Ila, pia kitamfaidi msomaji huria anayetafuta kitabu chenye burudani
kubwa kutokana na ucheshi, ushairi na uneni wa kupendeza.