Subiri Ndoa
Ujumbe ambao umo katika kitabu hiki unatueleza nguvu iliyo tendo la ndoa ikichanganuliwa vizuri kwa la Mungu na mifano halisi. Kutokana na nguvu isiyo ya kawaida maalumu sana ambayo hutokea pale ambapo tendo la ndoa hufanyika kwa mujibu wa kibali cha Mungu huleta faida kubwa sana kati ya wanandoa na kwa wale ambao hufanya tendo hili kabla ya ndoa (uasherati) au nje ya ndoa takatifu (zinaa), mashaka na hali ya kukosa utulivu kwa kuogopa fumanizi na pia nguvu iliyokinyume huzalishwa ambayo hupelekea mateso na hukumu ya Mungu kwa kumtenda dhambi, Pamoja na hasara nyingi ambazo kitabu hiki ulichonacho mkononi kinaeleza.
Kwa kuwa nguvu ya Tendo la ndoa husababisha Roho safi ya Muumba iatamie na kuitunza ndoa hivyo ni vema kumpa Mungu nafasi katika hatua za mahusiano mpaka ndoa takatifu ili kufurahia nguvu ya tendo la ndoa kama Mungu alivyokusudia tangu mwanzo wa uumbaji, na pia vijana wa kike na kiume ni vizuri na haki kabisa kujiepusha kabisa kutenda tendo hili au kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi yenye kuchochea kutenda tendo hili kabla ya wakati wake.