SEXUS: Siri za Ngono Tamu
Hivi unajua ni kwanini maneno Uchi, Uchizi na Uchawi yanashabihiana? Kitabu hiki kilipotoka kwa mara ya kwanza mwaka 2004 kilishutumiwa vikali na wananchi, viongozi wa dini na wanasiasa kwamba kilikuwa kinakiuka maadili. Viongozi wa dini walisema ngono iliwekwa kwa minajili ya kuzaliana tu, si vinginevyo. Rais akaagiza kitabu kifungiwe na mwandishi akamatwe.
Lakini kwanini?
Kitabu hiki sio cha kiponografia, bali ni mwongozo wa kitabibu juu ya mbinu za asili za wapenzi kuweza kuridhishana kitandani, kufanya mapenzi yao yaendelee kuwa mapya na matamu kila siku sanjari na kuzishinda kwa njia za asili changamoto zote za kingono kama vile wanaume kuwahi kufika kileleni, upungufu wa nguvu za kiume, wanawake kuchelewa au kushindwa kufika kileleni, kukaza uke pamoja na matiti yaliyolegea na masaibu mengine mengi yanayohusiana na ngono.
Sote tunajua kwamba kufeli kwa mambo chumbani huwa ni chanzo cha sintofahamu na kuanza kusalitiana katika mapenzi.
Ngono ni mchezo, na kila mchezo una siri na kanuni zake. Kitabu hiki ni Tiba ya Chumbani.