Ushindi katika hali ngumu
Kukata tamaa, machozi na uchungu hugeuka kuwa mavazi kwa mtu anayepitia hali ngumu. Tabasamu hupotea na furaha huwa kama kutafuta maji jangwani. Kiu kubwa huwa ni kuibuka mshindi lakini, Je! unawezaje kuibuka mshindi katika hali ngumu?.
Kitabu hiki kimejibu swali hili kinaganaga ili kumpa msomaji maarifa muhimu ya kujitengenezea ushindi apitapo katika hali ngumu. Watu wengi wapitapo katika hali ngumu hujikuta wapo peke yao; hakuna mfariji, wala watu wa kuwatia moyo. Kitabu hiki kitakuwa mfariji na mtu wa karibu kukutia moyo.
Kitabuni, mwandishi ameandika;“Usiruhusu hali ngumu kukuondolea furaha yako. Moyo wako usijazwe na huzuni kabisa kwa sababu ya ugumu wowote katika maisha…Ieleweke kuwa hakuna hali ngumu isiyo na uzuri. Hakuna hali ngumu isiyo na jambo la kujifunza… Raha ya kushinda changamoto ni kubwa kuliko raha ya kukosa changamoto. Uwezo wa kuyakabili mazingira huongezeka kwa kadiri tunavyoshinda hali ngumu tunazokutana nazo. Utamu wa stori si maneno bali ni ushindi kwenye magumu”
Basi, unaposoma kitabu hiki mpaka mwisho, kiu ya ushindi ikazaliwe ndani yako na uanze kujitengenezea ushindi ukiwa bado katika hali ngumu. Hali ngumu ni chakula cha washindi!