Hitimu kabla ya kuanza chuo
Kwa namna moja au nyingine kila mmoja wetu ambaye amepita au anategemea kupita chuoni atakubaliana na mimi kuwa kipindi cha maisha ya chuo kimejawa na changamoto nyingi sana za kimaamuzi, kiuchumi, kimahusiano, kihisia, na kifikra. Kubwa kabisa mara baada tu ya kumaliza chuo kila mmoja alikutana na mlima mwingine wa changamoto za maisha, ajira, kazi na ujasiriamali.
Ni tumaini langu kwamba ukiwa na mtazamo sahihi kabla ya kuwa chuoni, ukiwa chuoni na baada ya kumaliza chuo utaweza kufanya maamuzi sahihikwa wakati sahihi ili kuzishinda changamoto hizi. Kitabu hiki kinakupa mwanga wa maisha kabla ya chuo, maisha ya chuoni, na maisha baada ya chuo. Zaidi sana kinauweka mtazamo wako ufikirie zaidi ya lengo la kupata elimu ukiwa chuoni na hata baada ya kumaliza chuo kinauelekeza mtazamo wako kuitumia elimu uliyoipata chuoni kama nyenzo tu ili kuzifikia ndoto zako na kuwa tofauti na wengi ambao wameifanya elimu walioipata kuwa ndiyo ndoto yao wakasahau kuwa elimu ni nyenzo tu.
Kumbuka chuo sio hatima yako bali ni njia ya kuifikia hatima yako. Ajira sio hatima yako ni nyenzo ya kufikia hatima yako.