Mwongozo Halisi wa Mabadiliko Chanya
Kitabu hiki mwongozo halisi na madhubuti kwa mtu yeyote mwenye shauku ya kuona maisha yake yanabadilika katika hali chanya.
Zipo kanuni , mbinu muhimu, misingi na hatua za kuzingatia, vitu vya kufanya na vya kuacha vingine vya kupunguza ili uone maisha yako katika huu mwaka yanabadilika jumla katika hali chanya na uwe na uhakika wa kesho njema.
Mabadiliko chanya yana mkondo wake maalumu kwa mtu aliyetayari na mwenye kiu na anauwezo wa kulipia gharama zinazotakiwa Kuwa na mabadiliko chanya iwe katika ukuaji chanya katika Roho, Ujenzi wa fikra chanya na Kuwa na mabadiliko chanya katika mwili na mambo mengine kiuchumi n.k
Changamoto ni kwamba watu wengi wanapenda kuona Maisha yao yawe na mabadiliko chanya lakini hawapo tayari kulipa gharama za mabadiliko chanya, lakini wengine wanalipa hizo gharama kama kutafuta maarifa kuambatana na watu sahihi, matumizi mazuri ya muda lakini hawatumii ipasavyo maarifa waliyonayo kuwaletea mabadiliko chanya. Ukisoma hiki kitabu utapata nyenzo zote sahihi za kukuwezesha kutenda ipasavyo kwa ajili ya mabadiliko chanya.
Mara zote waliotayari kulipia gharama za mabadiliko chanya na kufanyia kazi maarifa haya ndio wanaozidi kuona mabadiliko chanya katika maisha yao.
Ndani ya kitabu nimeeleza
- Maana halisi ya mabadiliko,
- Aina za mabadiliko chanya na hasi,
- Utambuzi wa mwanadamu aliyekumbwa na Roho, Nafsi na mwili ili uweze kujua Sehemu sahihi ya kuanza kufanyia kazi kwa ajili ya ustawi wa mabadiliko chanya,
- Mbinu za msingi kukuletea mabadiliko chanya,
- Namna maarifa yatakavyokuwa nuru kukuletea mabadiliko chanya,
- Hatua za kufuata kukuletea mabadiliko chanya.
- Kujitathimini.
Pamoja na mtazamo wa mwandishi kuhusu Mafanikio na mabadiliko chanya.
Usiache kupambanua maisha yako kwa asilimia mia kwa ajili ya ustawi wa mabadiliko chanya katika maisha yako.
Unaposoma kitabu hiki utagundua kwamba, mwandishi anaweka msingi na nyenzo halisi za mabadiliko chanya na yenye uhakika wa maisha ya kesho yetu.