Tanuri la Furaha
Nini kifanyike ili kila mmoja wetu afurahie maisha, nini wajibu wa kila mmoja wetu katika kufanya dunia kuwa mahali bora pa kuishi? Maswali haya mazito ndiyo yamenisukuma kuandika siri 44 za kufurahia maisha.
Katika
kitabu hiki masuala ya kimwili, kiroho, kiakili yameguswa na namna ya kuweza kuwianisha
kwa usahihi ili mtu aweze kupata fu raha anayostahili.
Kamwe
hutojutia kukisoma kitabu hiki mwanzo hadi mwisho na hakika ni kwamba nasaha,
siri, na kanuni zilizowekwa humu zitakufaa sana kwenye maisha haya. Watu walio
wengi wamesaidika kupitia kusoma vitabu, kupokea ushauri na kupitia makala
mbalimbali.
Uzoefu
wangu wa mazingira ya kazi, elimu ya menejimenti ya rasilimali watu, maisha
yangu katika mtaa, ufundishaji katika shule mbalimbali, uandaaji wa mada za
stadi za maisha mtandaoni na ushauri kwa watu mbalimbali; ni vitu ambavyo
vimenisaidia sana kuandaa kitabu hiki na uhalisia wa maisha umeguswa kikamilifu
kwa lugha ya kueleweka.
Kitabu hiki kimewekwa katika muundo wa sehemu
kuu nne ambazo zimejikita kueleza furaha yenyewe ilivyo; siri za furaha,
uendelevu wa furaha kwa kuwa leo laweza kujitokeza hili na kesho likaibuka lile
na mwisho ni maoni na uzoefu wa watu mbalimbali juu ya furaha.