Kuenenda Kwa Kuukomboa Wakati
Waafrika wengi hatuna utamaduni wa kuheshimu muda tulionao. Na wakati mwingine tunaweza hata kuulinganisha muda na vitu vingine tunavyovimiliki. Lakini tunashindwa kuelewa kuwa muda ni rasilimali ambayo huwezi kuilinganisha na chochote, thamani yake haiwezi kurudishika kwa gharama yoyote.
Kupitia kitabu hiki cha "kuenenda kwa kuukomboa wakati", mwandishi ameeleza kwa upana sana kuhusu rasilimali hii adimu. Katika kitabu hiki utajifunza juu ya ukweli kuwa kila jambo lina wakati wake, kwa nini tutumie muda wetu ipasavyo, utajifunza faida za kutumia muda vizuri, utajifunza kwa nini ufanye kila jambo kwa wakati wake na mengine mengi utajifunza katika kitabu hiki cha "KUENENDA KWA KUUKOMBOA WAKATI." Elewa mafanikio yanayopatikana kwa wale wanaoheshimu muda na kuutumia ipasavyo.