Jirani Yangu
Jirani Yangu ni moja ya vitabu ambavyo vimelenga kuchochea mahusiano baina ya watu wanaoishi katika maeneo jirani. Pia ni kitabu ambacho kimefafanua kwa undani zaidi kuhusu jirani, na kimeeleza wajibu wa mtu kwa jirani yake, lakini pia kimeeleza jinsi gani mtu hasa aliyeokoka anavyoweza kuishi na watu ambao hawajaokoka na bado ikawa ni kwa utukufu wa Mungu, kwa sababu ya ule upendo wa kimungu ulio ndani yake.
Kitabu hiki kimebeba majibu mbalimbali kwa ajili ya kujibu maswali ambayo watu wengi wamekuwa wakijiuliza, kwa mfano yule mwanasheria aliyemuuliza Yesu afanye nini ili aurithi uzima wa milele? Jibu la Yesu ndiyo asili ya kitabu hiki na jibu hilo ingawa mwanasheria yule lilikuwa kama lisilomfaa lakini sisi linatufaa sana na tunapaswa kulielewa jibu lile kwa undani. Ili tulielewe kitabu hiki kimekuja kwako. Usikubali kikapita tu kwako.