Kiongozi Mtumishi
Katika kanisa la leo, dhana ya uongozi wa kiutumishi inaporomoka kwa kasi. Tuna viongozi wengi, lakini tuna viongozi watumishi wachache. Hitaji kubwa la kanisa leo sio viongozi tu, bali viongozi watumishi. Falsafa ya uongozi aliyotuachia Yesu Kristo miaka zaidi ya 2000 iliyopita ya kuwa kiongozi ni mtumishi inatekelezwa kwa udhaifu sana.
Viongozi wengi sio watumishi tena bali ni watumikiwa. Hawapo kutumikia tena wapo kutumikiwa.
Katika kitabu hiki, mambo muhimu kuhusu Uongozi wa kiutumishi yamefundishwa, nayo yatabadilisha kabisa mtazamo wako kuhusu uongozi.
- Maana ya utumishi
- Utumishi katika maisha ya Yesu Kristo
- Uongozi wa kiutumishi na misingi yake
- Uongozi usiofaa usio wa kiutumishi
- Kanuni za uongozi wa kiutumishi
- Tabia za kiongozi mtumishi