Ushauri wa Afya ya Akili
Afya ya akili ni mada tata ambayo imekuwa ni changamoto inayo athiri watu wengi kwenye nyanja zote za maisha. Leo hii matatizo ya afya ya akili na magonjwa ya akili yanayo ongezeka sana na kuwa ni kawaida katika jamii. Ni uhalisia wa kweli kwamba mtu yeyote yule anaweza kuwa kupitia changamoto na mapambano ya afya ya akili.
Ili kuepukana na mtazamo potofu unaozunguka masuala ya afya ya akili katika jamii, tunahitaji kuweka kipaumbele katika elimu na ulewa sahihi kwa kujielemisha wenyewe na wengine juu ya uhalisia wa changamoto za afya ya akili, magonjwa ya akili, matibabu mbadala yaliyopo na athari ambazo zinaweza kuwepo juu ya maisha ya watu.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtazamo wa kibiblia na kisaikolojia na utapata fursa ya kujifunza mambo mengi kuhusu afya ya akili na hisia, kama vile, uhusiano wa afya ya akili na afya ya mwili, sababu na vyanzo za matatizo ya afya ya akili, dalili mbalimbali za matatizo ya afya ya akili, aina za magonjwa ya akili, kinga na tiba dhidi ya matatizo ya afya ya akili na jinsi ya kuwapa huduma ya kwanza ya ushauri wale wanaopitia changamoto ya afya ya akili.