Vita ya Baraka (The War of Blessings)
Kitabu kinaelezea namna gani siasa hujificha ndani ya dini na vile ambavyo dini hujificha kwenye siasa ili kuvipiga vita vyema, vita vinavyo muwezesha mwanadamu kuutawala ulimwengu kwa mfano wake Mungu, kitabu kinamuhusu kila mtu mwenye dini na yule asie na dini lakini wote wamefungiwa katika mfumo wa maisha ambao mamlaka ya nchi ndio haina dini. kitakufungulia milango ya "KUTOKA" (hijira, exodus) na kisha kukupatia njia za kuyafikia maendeleo ama kukupatia mafanikio ya kweli.
Hii ni sehemu ya kwanza ya kitabu VITA YA BARAKA (The War of Blessings) vilivyoanzishwa na tukio la Ibrahimu na mwanae wa pekee, na ni kitabu kitakachoweza kuakisi matendo yako yote ya kimwili yakamilishwe katika roho, na msingi narejeo yake hasa upo katika Qur'an na Biblia.
Na kisha mafanikio ya kukamilishwa huko kimwili na kiroho kuwa ndio jibu la migogoro ya ndani ya nafsi yako mwenyewe, migogoro ya ulimwengu wa wanawake na wanaume, dhehebu moja la dini lisiwe dhidi lingine, ndio itakua sababu ya utangamano imara wa Tanganyika na Zanzibar na kisha Afrika yote, kuishi katika mseto au utangamano wa baraka ya UBEPARI usio dhidi ya baraka ya UJAMAA wa kiafrika. na utangamano huo pekee ndio utaweza kukufanikishia kuwa na katiba (written au unwritten constitution) itakayokupatia mamlaka kamili katika kila ngazi ya maisha yako na kukufanya kuwa kiongozi imara mwenye mfumo imara wa maisha. Kitabu kinaielezea Afrika kama nchi kupitia matukio ya maisha na watu wake katika eneo la Afrika Mashariki hususani Tanzania.